Home » Archive for Julai 2015
Omondi kuzivunja mbavu za wakazi wa Dar Jumamosi hii
Onyesho hilo ambalo limeandaliwa na CDEA:“Culture and Development East Africa” kwa kushirikiana na Nafasi Art Space litafanyika jumamosi ya tarehe moja mwezi wa nane mwaka huu, kuanzia saa moja jioni mpaka asubuhi katika ukumbi wa Nafasi Art Space-Mikocheni.
Mratibu wa onyesho hilo Naamala Samson alisema kuwa mbali na onyesho hilo pia kutakuwa na burudani kemkem kutoka kwa maDJ wa Santuri Safari kutoka Kenya na Uganda.
“Wanamuziki wote wamefanya mazoezi ya kutosha na wamejiandaa kikamilifu kwa onyesho hili la kihistoria, ni siku hiyo watanzania watapata fursa ya kuonja ladha ya muziki wa Afrika Mashariki wenye vionjo vya nyumbani na kupata vichekesho vya mwaka kutoka kwa Omondi,” alisema Naamala.
Bendi ya Sarabi ni miongoni mwa bendi kubwa na zinazofanya vizuri nchini Kenya na kuwepo kwake kwenye tamasha hili kutanogesha mambo na kutoa burudani ya kutosha kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani.
Bila P-Funk, Marco Chali, Pancho nisingeiva kama producer – Dully Sykes
Dully Sykes amemtaja producer wa Bongo Records, P-Funk Majani kuwa ni miongoni mwa watu waliomfundisha mambo mengi kuhusiana na utayarishaji wa nyimbo.
Dully aliwahi kumiliki studio iitwayo Dhahabu Records kabla ya kuanzisha nyingine 4.12 iliyopo hadi sasa ambapo yeye mwenyewe ndiye producer.
“Namshukuru sana P-Funk maana yeye ndo kati ya maproducer walionisaidia na kunifundisha hata kugonga kick na snare,” Dully aliiambia E-News ya EATV.
“Alikuwa ananiambia kuwa kiCi inatakiwa KUWA katika level ipi ili muziki usikike vizuri, yaani namshukuru amenifundisha vingi. Na mtu kama Marco Chali alikuwa sio mchoyo kunipa vitu. Namshukuru pia Pancho ni mdogo wangu nimemlea mwenyewe na Producer Mbezi, hawa ni wadogo zangu wamenisaidia sana.”
Exclusively video mpya ya Mayunga, mshindi wa Airtel Trace Music Star kurushwa Trace Urban Ijumaa hii
Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star, Mtanzania Mayunga Malimi anategemea kuachia video yake mpya ‘Nice Couple’ ambayo itaoneshwa kwa mara ya kwanza na kituo cha Trace Urban cha Ufaransa Ijumaa hii July 31.
Mayunga ambaye alienda Afrika Kusini kushoot video hiyo, amewataarifu mashabiki wake Kupitia ukurasa wake wa Intagram.
“Aya wadau wangu jumlisha na manice couples watoto kwa wa kubwa wimbo wenu una dondoka kesho kwenye kituo cha trace tutupie macho ili kuweza kuona kazi ya kijana wenu hop mtafurahia asanteni na nawapenda sana.”– Mayunga
Kupitia shindano la Airtel Trace Music Star ililofanyika mapema mwaka huu, Mayunga alishinda mkataba wa kurekodi muziki na label ya Universal Music wenye thamani ya $500,000.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)