Akizungumza katika moja ya fursa ya kijamii nchini |
MAFANIKIO siku zote huanza kujengwa na fikra
zilizo imara ndicho kitu kinachomfanya Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini
kutoka katika kundi la weusi,Nickson Saimoni maarufu kama 'Nickk Wa Pili'
kuzidi kuwa nyota inayong'ara kwa wasanii wengine nchini.
Kama ilivyowazi kuwa msanii huyu ni msomi ambaye
amefanikiwa kushiriki katika fursa mbalimbali za kijamii ambazo anaamini
zimechangia kumkuza zaidi kiakili na kutambua uhalisia wa maisha ya mtanzania
kuliko alivyosoma darasani.
Baada ya kumaliza elimu ya shahada katika chuo kikuu cha Dar es salaam |
Historia yake
Nickk wa pili alizaliwa katika hospitali ya Maunt
Meru mjini Arusha na kuoma elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Arusha
kidato cha kwanza mpaka cha nne na kumlizia Kigoma kidato cha tano na sita na
kujiunga elimu ya juu katika chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka 2007.
Alipenda na akijua kuimba muziki tangu akiwa
elimu ya sekondari na kupata umaarufu akiwa mwaka wa pili chuo kikuu cha Dar es
salaam mwaka 2008 baada ya kushirikishwa katika wimbo wa Joh makini ujulikanao
kama 'Niaje Nivipi'.
Bada ya kujulikana alianza kutambulisha kazi zake
zikiwemo Good Boy aliyofanya na Msanii maarufu wa Rnb nchini Rama D na wimbo
ujulikanao kama 'Higher' aliofanya mwandaaji Pancho Latino na alimshirikisha
Joh makini.
Hakuishi hapo aliendelea kufanya vibao vingine vingi
vikiwemo 'Bum Kubam' aliyomshirikisha
G-Nako, Sitaki kazi aliyomshirikisha Ben Pol na Joh Makini bila kumsahau
G-Nako.
Kazi zingine alizofanya ni kitu changu kizuri
aliyomshirikisha Lina,hatuendani aliyomshirikisha Belle 9 na Kiujamaa
aliyomshirikisha Pipi.
Akiwa na kundi lake la weusi |
Anauchukuliaje uwezo wa msanii G-Nako kutokana na
kumshirikisha nyimbo nyingi.
Nikk Wa Pili alisema kuwa G-Nako ni msanii
mwaenye ufundi na uwezo wa hali ya juu na mara nyingi huwa wanakuwepo pamoja
studio anaporekodi ndoyo maana mara nyingi wanafanya kazi pamoja.
Kama ilivyo wazi ni kwamba wasanii hawa mbali na
kuwa kundi moja pia wamefanya kazi kadhaa kwa kushirikiana zikiwemo 'Pea',Bum
Kubam,sitaki kazi,Mavijana.
Mtazamo wake kwa kundi la muziki la weusi
Kundi hili lililoundwa na wasanii walikuwa katika
makundi ya River Camp Soldier na Nako 2 Nacko ,linaundwa na wasanii watano
ambao ni, G-Nako,Joh Makini,Bonta,Lord Eyes na yeye mwenyewe Nick Wa Pili.
Nick Wa Pili anasema kuwa kampu ni weusi ipo kwa
ajili ya kutengeneza muziki mzuri nchini na tayari hatua zinafanyika na
washabiki wa muziki wao wanafurahia.
Alimtaja msanii ambaye ni kioo na mwongozo wake
nchini na nje.
Nick Wa Pili hakusita kumtaja msanii maarufu wa
Hip Hop nchini,Joh Makini kuwa ni taa na mongozo wa muziki wake.
"Joh Makini ni msanii mkongwe mwenye uwezo
wa ajabu na wa juu sana katika wasanii nchini".Alisema Nickk Wa Pili.
Aliongeza kuwa kwa upande wa nje anamkubali
msanii wa mashuhuli duniani ajulikanaye kama 'Jaz Z'.
Alifunguka kuhusu producer Nah reel
"Nah Reel ni mwandaaji maarufu wa muziki
anayejua kwenda na wakati anafanya muziki unaopendwa na mashabiki kila
kukicha".Alisema
Aliongeza kuwa licha ya muandaaji huyo kuwa mtu
wa karibu(rafiki) lakini anaamini kila mtu anaujua vizuri uwezo wa mwandaaji
huyo ambaye alifanya naye kazi akiwa studio za Kama kawa Record,Home Town
Record na sasa katika The Industry ambako kote alifanya kazi zilizopenda na
mashabiki wa muziki wake.
Akizungumzia programu ya fursa ya Clouds Media
Nickk Wa Pili alisema kuwa programu hiyo
ilimfanya kufanya utafiti wa maisha halisi ya mtanzania kitu ambacho hata
darasani hakufundishwa.
Nickk Wa Pili alieleza kuwa programu hiyo ilikuwa
na lengo la kuhamasisha vijana na kupata ushuhuda wa kujifunza kutoka kwa watu
waliofanikiwa iliyokuwa safari ya kuzunguka mikoa yote nchini.
Matatizo/changamoto
Nick wa Pili anasema kuwa muziki wetu
unachangamoto kubwa kwani katika vyombo vyetu vya habari nchini unachezwa
muziki usio na viwango hali inayofanya muziki mzuri nchini kutopewa thamani na
kuonekana mbaya.
Ineandaliwa na Sylvester David
Email:muzikibegani@gmail.com
Call:0715577805 au 0768538085