Ivan Ssemwanga, aliyekuwa mume wa Zari The Bosslady na aliyezaa naye
watoto watatu ameanza kurusha mashambulizi kwa adui yake namba moja,
Diamond Platnumz.
Mfanyabiashara huyo mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini huenda
akalipiza kisasi kwa Diamond anayetarajia kupata mtoto wake wa kwanza
kutoka kwa Zari kwa mbinu ya ‘jino kwa jino’ ama zile za ‘kama noma basi
iwe noma’.
Picha liko hivi, Wema Sepetu kumbe yupo nchini Afrika Kusini ambako hata
hivyo hatufahamu ameenda kufanya nini. Mshkaji wa karibu wa Ivan, King
Lawrence (Yule mchizi aliyempa ofa Diamond ya $40,000 ili aachane na
Zari), ameshare picha kwenye mtandao wa Instagram akila bata na Wema
huku Ivan akiwpo pia.
Kuanzia Kushoto: Wema, Ivan na Lawrence akiwa na demu wake
Kwenye picha hizo, Lawrence anaonekana akiwa amekaa juu ya mapaja ya
msichana asiyejulikana na pembeni yake yupo Ivan huku Wema aliyevaa
kigauni kifupi cheusi akiwa kulia kwake.
Lawrence pia amepost video kadhaa akiwa kwenye club hiyo na kuziandika
ujumbe wa mfumbo ambao unaeleweka wazi kuwa unawaendea Zari na Diamond.
“Rich Gangstas – What goes around comes around,” ameandika. “Oh Z*** get
out of the way,” ameandika kwenye video nyingine ambayo unasikika wimbo
wa Ludacris, Move Bitc*.
Awali Lawrence alipost picha nyingine hiyo chini akiwa kwenye eneo lile lile ambalo Wema alipiga picha.
Ni mapema sana kuhitimisha kuwa Ivan anataka kulipiza kisasi kwa Diamond
kwa kumchukua Wema, lakini ni wazi kuwa kambi yake inataka kupeleka
ujumbe ulio wazi kwa Chibu kuwa ‘vita imeanza’.
Acha project iendelee…
SOURCE : BONGO5.COM