Producer Nah Reel akiwa studio
NA SYLVESTER DAVID
MWANDAAJI maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini,Emanuel Mkono‘Nah Reel’amekiri kuwa na uwezo mkubwa katika uandaaji wa muziki kutokana na kazi alizozifanya na wasanii mbalimbali wakubwa nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na MUZIKI BEGANI kuhusu mabadiliko ya muziki nchini,alisema mabadiliko ni makubwa sana na yuko katika hatua za kuleta muziki mzuri katika soko la muziki nchini.
Nah Reel ambaye ni mwandaaji aliyefanya kazi katika studio za Kama Kawa Record,Home Town Record,Switch Record na sasa katika studio yake ijulikanayo kama ‘The Industy’.
Aliwataja wasanii aliofanya nao kuwa ni wengi wakiwemo Kundi la Weusi,Vanessa Mdee, Diamond Platnum,Bonta,Kundi la Navy Kenzo,Izzo Busness,Kundi La Pah One,Mwana Fa,Roma,Kalla Jelemaya,Baba Levo,Rama D,Mapacha(Maujanja Suplayaz),Gosby,Quick Racka na Shilole.
Pia aliwataka mashabiki wa muziki wake nchini wategemee kazi nzuri na zenye ubora kutoka kwake na studio yake ya ‘The Industry’.
PICHA ZA BAADHI YA WASANII ALIOWAHI FANYA NAO KAZI
QUICK RACKA
DIAMOND
IZZO BIZNESS
SHILOLE
VANESSA MDEE
0 Response to "NAH REEL:KUFANYA KAZI NA MASTAA KIBAO NCHINI NI KIPIMO CHA UWEZO WANGU "
Chapisha Maoni