Producer Sappy ndiye Producer ambaye aliproduce ngoma Namba Moja kwenye Chart za 20 Bora za Mambo Jambo Radio Arusha kwa wiki iliyopita XO ya JOH MAKINI.
Huyu ni kijana wa Kitanzania ambaye amejipatia Umaarufu wa Kupika Midundo ya Tofauti sana ya Muziki hapa Afrika Mashariki. Sappy amefanya kazi na Wasanii Kibao hadi sasa Kama Prezzo ambaye alimuundia ngoma ya Marry Marry na My Girl, Kafanya Kazi na Kaka Sungura Rabbit, Nazizi na Wasanii wengine Kibao wa Kenya.
Heshima Kubwa sana aliipata kupitia ngoma ya Budder than Most ya Redsun ambayo Remix yake alishirikishwa Mkali Demarco toka Jamaica na sasa Heshima ya Sappy kwa Tanzania imeongezwa na XO Ngoma kali toka kwa joh Makini akishirikishwa Baba Samantha GNako.
Pichani ni Joh Makini & Sappy
Akiongea na @DJHAAZU ndani ya Kipindi cha Dundo cha Mambo Jambo Radio Mapema Leo Sappy ameelezea Historia yake hadi kuja Kufanya kazi na Weusi wasanii ambao anasema Alikuwa na ndoto ya kufanya nao Kazi toka kitambo sana.
Sappy alienda Kenya Kusomea Muziki akiaamini kuwa Muziki unahitaji Elimu zaidi ya ambavyo watu wanafikiria na Alivyoenda Kenya Kusoma akagundua kuwa Muziki Unavyofanywa Kenya unafanywa Kisomi Zaidi tofauti na Tanzania.
Katika Mazungumzo yake akatiririka Mengi haswa alivyokuwa akitamani Siku moja afanye Kazi na Vijana ambao anaamini Wanajitambua na wanajua wanachokifanya WEUSI
Pichani ni Sappy akiwa na Redsun
Prezzo & Sappy
PATA NAFASI YA KUMSIKILIZA KWA KU-CLICK LINK HII HAPA:- PRODUCER SAPPY KENYA KUNA KITABU CHA MUZIKI ….BY @DJHAAZU