Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia January Makamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni ya na kampuni ya Copyrights Management East Africa Limited (CMEA).
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo yenye lengo la kuwakwamua wanamuziki katika umaskini. CMEA pia itawawezesha pia
watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.
Mwanamuziki Mkongwe nchini, John Kitime akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni ya inayojishughulisha na Hakimiliki za kazi za wasanii katika nchi za Afrika Mashariki ijulikanayo kwa jina la Copyrights Management East Africa Limited (CMEA).
…………………………………………………………………………………………..
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewataka wanamuziki nchini kuachana na kutegemea kupata shoo za majukwaani na kupata umaarufu usiokuwa na tija kwa kujiunga na kampuni ya Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) ambayo inasimamia haki miliki za kazi za wasanii wa ukanda wa nchi ya Afrika Mashariki.
Naibu Waziri Makamba alisema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa kampuni ya CMEA ambayo ipo chini ya mtayarishaji wa muziki maarufu, Paul Matthysse (P-Funk) ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kamuni hiyo.
Makamba alisema kuwa wanamuziki wengi nchini wanapata umaarufu mkubwa wa bila kipato kutokana na kazi zao bora kwani hawafaidiki na utunzi wa nyimbo zao zinazopigwa kwenye televisheni na vituo vya redio mbalimbali.Alisema kuwa matokeo yake wanapotea katika fani hiyo na kuwa maskini maarufu na faida kubwa kwao ni kupata sifa kwa warembo mbalimbali ambao huwakimbia pale wanaposhuka katika fani.
“Mimi najua muziki na wanamuziki, hakuna mtu anayeweza kunidanganya, wanamuziki wanapata tabu katika utunzi na baadaye kutafuta fedha za kurekodi kwa kukopa au kwa kuombaomba, baadaye watafute fedha za kuwapa madj wa redio na wa vipindi vya televisheni ili wimbo wake uchezwe na kupata shoo mbalimali kwa kipato kidogo,” alisema Makamba.
Alisema kutokana na hali ilivyo, mwanamuziki anaishia kukuapata shoo kwa ujira mdogo na akipotea katika fani, anakuwa maskini maarufu.
“CMEA ni sululisho kwenu, kampuni hi itafanyakazi pamoja na Chama Cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) kuweza kujua wimbo wako au video yako imechezwa mara ngapi redioni au kwenye televisheni na unastahili kulipwa shilingi ngapi,” alisema.Alisema kuwa hata baada ya kuacha muziki, utaendelea kupata fedha ‘pensheni’ kutokana na wimbo au video yako kuchezwa redioni na kwenye televisheni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse alisema kuwa mbali ya wanamuziki, kampuni yao itawawezeha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.
Matthysse alisema kuwa kampuni yao imewekeza mitambo ya kisasa inayowezesha kuchapisha na kuhakiki nyimbo pindi zinapochezwa hewani na televisheni na redio na kutoa ripoti za aina mbalimbali zinazohitajika kutumika kwa malengo maalum.
“Pia tunapokea na kuhifadhi nyimbo kwenye mitambo maalum kwa matumizi ya uhakiki, na kudhibiti kiasi cha mirabaha ambacho Cosota kupitia vyombo vya habari inatakiwa kuwalipa wasanii kulingana na idadi kamili ya urushwaji wa kazi zao,” alisema Matthysse.