Baada ya uvumi kusambaa kuwa mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi Vengu amefariki na baadae kaka yake alikanusha uvumi huo, kiongozi wa kundi hilo Sekioni David
amesema wamepata usumbufu mkubwa juu ya uvumi huo na wao kama kundi
wameamua kuchukua hatua zaidi ili kukomesha tabia hiyo kwa kuwa sio
mara ya kwanza, wamepata ushauri kutoka TCRA ambao wamewashauri kuchukua
hatua ili kuweza kujua chanzo cha uvumi huo na kuchukua hatua zaidi kwa
wahusika na muda sio mrefu mhusika atajulikana
Kuhusu Afya ya Vengu
amesema ni mzima ila kutokana na ushauri wa daktari anatakiwa awe
kwenye utulivu ambao unamfanya awe nje ya kundi lakini yeye bado ni
mfanyakazi na anaendelea kulipwa kama kawaida.
Ilikusikiliza story zote bonyeza play hapa chini…