Mahakama ya Rwanda Ijumaa iliyopita ilimhukumu mwanamuziki maarufu wa nchini humo, Kizito Mihigo kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la kupanga njama dhidi ya serikali ya Rwanda ikiwemo mipango ya kumuua Rais Paul Kagame na maafisa wengine wa juu.
Kizito Mihigo
Mihigo alipatikana na hatia ya kuanzisha kundi la kihalifu na njama ya kutekeleza mauaji japo jaji alitupilia mbali makosa ya kuhusika kwenye vitendo vya kigaidi.
Mihigo, 35, aliyekanusha madai yote ni mhanga wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.
Waendesha mashtaka walidai kuwa msanii huyo alihusika kukusanya vijana kwaajili makundi ya waasi wa Kihutu ya RNC na FDLR.
Mihigo ni maarufu mno nchini Rwanda kwakuwa alikuwa akitumika zaidi kuimba wimbo wa taifa kwenye hafla za kiserikali zikiwemo zile ambazo Rais Kagame alihudhuria
http://www.bongo5.com