Vanessa Mdee ameungana na wasanii wengine wa Afrika Mashariki wakiwemo Juliani wa Kenya, Emmanuel Jal wa Sudan na Syssi Managa wa Congo Brazzaville kwenye wimbo wa kampeni maalum dhidi ya mauaji ya tembo iitwayo, Ndovu Zetu. Kuanzia kushoto: Syssi Managa, Emmanuel Jal, Vanessa Mdee na Juliani
Pia wasanii hao pamoja na kundi la Sauti Sol walitumbuiza kwenye Ndovu Zetu Concert kwenye viwanja vya burudani vya umoja wa mataifa jijini Nairobi.
Wasanii hao walishoot video ya wimbo unaohamasisha ulindaji wa wanyama husasan tembo. Wimbo huo unaitwa Tusimame.