NEWZZZ:Fid Q kuwasharikisha Sauti Sol kwenye joint yake mpya



Fid Q, AY, Shaa na Sauti Sol wakiwa studio
Msanii nguli wa muziki wa hip hop nchini  Fid Q amewashirikisha sauti sol katika kibaochake kipya kitakachokuja hivi karibuni.

Akiongea jana kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Citizen Radio ya Kenya, Fid amedai kuwa wimbo huo wameurekodi juzi usiku.



“Nilikuja Nairobi kwaajili ya kurekodi na Sauti Sol, namshukuru Mungu tumefanya session last night na kiukweli wote tumeondoka happy,” Fid alimwambia mtangazaji wa kipindi hicho, Mzazi Willy Tuva.

“Naposema hivyo namaanisha kuwa tumefanya ngoma fulani hivi ambayo wengi hatukuitajia kama ingekuwa nzuri hivyo. Ninachoshukuru ni ile chemistry ndani ya studio. Studio tulikuwa wengi kidogo kwahiyo tumejaribu kushare ideas kidogo, watu wasubiri kitu fulani ambacho kitakuwa amazing kidogo,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Fid alisema amepunguza spidi ya kuachia ngoma mara kwa mara kwakuwa amegundua nyimbo zake zinahitaji muda mrefu kueleweka kwa mashabiki wake.

Alidai kuwa amegundua kuwa nyimbo zake hazishuki chart na kwamba hata wimbo mmoja tu kwa mwaka unatosha.

Fid pia alizungumzia tatizo la wasanii wengi wa hip hop kushindwa kufanya vizuri na kusema kuwa wengi wanaimbiana wao kwa wao na sio kutoa nyimbo zinazogusa maisha ama hisia za mashabiki.

“Unakuta mtu anapiga labda ‘mimi sijui napita na metaphors kadhaa, sijui utaniambia nini’ sasa hiyo wale akina mama ambao wako uswahili kule hawaelewi tunaongea kuhusu nini,” alisema.

“Mara nyingi tunaimba ‘mimi ni mkali kuliko wewe, mimi ni noma, mimi ni nini’, kwahiyo inakuwa kama unawaambia wasanii wenzako, hauwaimbii wananchi. Inaeleweka kuwa ni mistari ya hivyo lakini sio album nzima,” alisisitiza.

“Kwahiyo unakuwa kama emcee wa battle. Unakuta mtu anaweza akashinda kwenye battle field lakini hawezi kutoa hit song. Na tukumbuke kwamba muziki upo kwaajili ya kuwaambia wananchi, kuwaambia watu, kwahiyo tuwaimbie watu, tuongee nao kuhusiana na vitu vinavyowahusu wao. Muziki kwa namna fulani lazima ureflect community kwa ujumla.”