Picha tofauti zikiwaonesha Jonny Evans na Papiss Cisse wakitemeana mate kwenye uwanja wa St James' Park. |
LONDON, England
BEKI wa Manchester
United Jonny Evans na mshambuliaji wa Newcastle United Papiss Cisse huenda
wakakabiliwa na kifungo hadi cha miezi sita endapo watapatikana na hatia ya
kutemeana mate.
Wawili hao
walinekana wakitemeana mate wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England jana
Jumatano usiku kwenye uwanja wa St James' Park.
Mwamuzi wa mchezo
huo Anthony Taylor alizungumza na Evans na Cisse baada ya tukio hilo la kipindi
cha kwanza, lakini hakuna aliyepewa kadi.
Hatahivyo, Chama
cha Soka cha England kinasema kuwa kinasubiri taarifa ya mwamuzi kabla ya
kuamua kama watachukua hatua yoyote.
Msimu uliopita, George
Boyd alifungiwa mechi tatu kwa kumtemea mate kipa wa Manchester City Joe Hart.
Wachezaji kadhaa
wazamani wanaamini kuwa Evans na Cisse wanastahili adhabu.
Kiungo wazamani wa
Newcastle Dietmar Hamann alielezea kuwa kitendo hicho "kamwe hakikubaliki".
Picha za
televisheni zilimuonesha Evans akimtemea mate Cisse, aliyekuwa chini.
Naye mshmabuliaji
huyo wa Senegal alionekana kutema mate upande wa Evans.
Sio kocha wa Newcastle
John Carver au mwenzake wa Manchester United Louis van Gaal aliyesema kama
aliona kitendo hicho.
"Siwezi
kusema lolote kuhusu hilo, " alisema Carver, ambaye timu yake ilifungwa
bao 1-0.