Mwanadada Chiku Ketto a.k.a Chiku K Balaa ameamua kuweka wazi hisia zake alizonazo kuhusu kile anachokiona kinamtesa Aliyekuwa Member Mwenzake wa Kundi la LaFamilia.
Akizungumza na Kipindi cha DUNDO cha MamboJambo Radio Arusha kupitia Kipengele cha DROP BOX Chiku amesema ana mpango wa kukaa Karibu zaidi na Chid Beenz Kwakuwa anajua anakoelekea sio kwema kwani wakati wakiwa Pamoja Chid alikuwa na Mafanikio na Hakuwa kama alivyokuwa Kitu ambacho kinaonekana kama Chid beenz amekosa mtu wakuwa karibu zaidi na yeye kwa Ushauri na Ukaribu wa Kimawazo Chanya.Bila shaka mmefuatilia pia Kesi ambayo ilikuwa inamkabili Chid Beenz ambayo ilikuwa ya Kukutwa na Madawa ya Kulevya Katika Uwanja wa JK Nyerere Airport na kuachiwa huru kwa Faini ya sh. 900 000/= za Kitanzania Hivi juzi hii ni moja ya sababu zinazoonyesha Chid Baanz amefikia kubaya zaidi.
UKIWA unakumbukumbu nzuri sana utakumbuka wakati ule chid akiwa na LaFamilia Team yake hata kiafya alikuwa Kajaza na hata watu walikuwa wanamuogopa kwa kuwa alikuwa na Lile Body Flani la Kinako ila kwa sasa hata machalii wanweza kumchezea Japo Wembamba hauna maana ya kuwa Umeisha na nguvu ila kiukweli Chid Amepungua sana Kiafya.