GARI LA KANUMBA LAGOMA KUTOKA SOKONI

GARI LA KANUMBA LAGOMA KUTOKA SOKONI


Gari la Kanumba Lashindwa Kuuzika Sokoni
Ikiwa ni miaka mitatu sasa imepita tangu aliekuwa staa wa Bongo  Movies, marehemu Steven Kanumba, inadaiwa kuwa gari alilokuwa akilitembelea aina ya Toyota Lexus lenye namba za usajili T750 AER limezidi kudoda sokoni.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti la Risasi kimepenyeza habari kuwa gari hilo lililonunuliwa na marehemu kwa shilingi milioni 78, linapatikana maeneo ya Msasani, jijini Dar kwenye jengo la mikopo ambapo linauzwa kwa bei chee ya shilingi milioni 18 hadi 14.
“Nilikuwa nikijipitia kukagua magari lakini ghafla nikakutana na gari la Kanumba. Sikuamini mpaka pale nilipoingia na kulipiga picha kisha nikaambiwa na thamani yake,” kilisema chanzo.Chanzo kiliendelea kutiririka kuwa huenda kuna mkopo ulichukuliwa na kuacha dokumenti zote za gari hiyo na iliposhindikana kulipwa gari hiyo ikapigwa mnada.
“Sidhani kama gari kali kama ile ipigwe bei ya milioni 18 tu, lazima kutakuwa na mkopo ambao haujamalizwa ndiyo maana limepigwa kiasi hicho cha pesa ili kukamilisha.”Awali ilisemekana kuwa gari hilo lilikabidhiwa kwa msanii wa filamu Bongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ ili alinunue kwa gharama ya shilingi milioni 40 lakini kwa kuwa liligundulika na matatizo mengi akawa tayari kutoa shilingi milioni 25 ambapo pia ilishindikana na kurudishwa kwa familia ya Kanumba.
Gazeti hilo lilimtafuta mama Kanumba, Flora Mtegoa ili kujua anazungumziaje gari hilo kudoda sokoni, alijibu:“Mimi sijui chochote kuhusu hilo gari naona mnazidi kuniumiza tu hapa naumwa, hata kama nimeuza au limefanywaje jamani maswali mengine yanaumiza hebu niacheni maana sijui kinachoendelea kuhusu hilo gari,” alisema Mama Kanumba.
WAFAHAMU MASTAA AMBAO SHAMSA FORD ANAWAKUBALI ZAIDI

WAFAHAMU MASTAA AMBAO SHAMSA FORD ANAWAKUBALI ZAIDI

Hawa Ndio Mastaa 10 Wakiume wa Bongo Movies  Ambao Shamsa Anawakubali
Staa mrembo wa Bongo Movies, Shamsa Ford ambae ni Binamu Wa Nay Wa Mitego amewataja hawa kua ndio wakali wake.

“Mambo vipi Tanzania? Leo ningependa kuwatajia wanaume 10 ambao huwa napenda sana uigizaji wao, haimanishi kwamba wao ndo the best kuliko wengine but napenda tu sanaa yao. (1) Single Mtambalike ‘Richie’ (2) Marehemu Adamu Kuambiana (3) Marehemu Kanumba (4) Muhogo Mchungu (5) Swebe (6)Tino (7) Gabo (8) Vincet Kigosi ‘Ray’ (9) Bishanga Bashaiga (10) Cloud112....nawakubali sanaaaaa kila mtu hapa ana radha yake”- Shamsa alieleza.
Hii ni kwa upande wake yeye.
DIAMOND:WEMA HATUKUENDANA TABIA ILIKUWA LAZIMA TUACHANE

DIAMOND:WEMA HATUKUENDANA TABIA ILIKUWA LAZIMA TUACHANE

Diamond: Ilikua ni lazima kuachana na Wema.STAA Bongo flava kwa sasa Naseeb Abdul Jumaa “Diamond plutnums”, amefunguka kuwa ilibidi aachane na Wema Sepetu ili maisha mengine yaendelee.
 
Kupitia mitikisiko ya pwani, Diamond amedai mara kadhaa alitumia nguvu nyingi kujenga mahusiano yake bila mafanikio, kwa kuwa yeye na Wema “Madame” hawakuendana tabia.
“Nafikiri hatukuendana tabia kwa kuwa nilifanya kila niwezalo, tulikubaliana kwa pamoja na ikafika hatua ikawa ni lazima tuachane tu” alifunguka Chibu “diamond”.

Kwenye line nyingine Plutnumz alithibithibitisha rasmi ujauzito wa kichuna wake wa sasa Zarrina Hassan “Zarri the boss lady”, na kumpa sifa mob kuwa ni mwanamke wa pekee aliyekubali kupata nae mtoto

“Mabinti wengi niliokua nao, na hata wa hapa mjini kukubali kua na mtoto ni jambo zito sana so nina kila sababu ya kumshukuru sana na nampenda kwa kweli” alimalizia Diamond.

ALI KIBA AITIKISA DAR LIVESHOW YA PASAKA

ALI KIBA AITIKISA DAR LIVESHOW YA PASAKA

Mwanamuziki Ali Kiba akizikonga nyoyo za mashabiki waliofurika Dar Live katika shoo yake ya Mwana Dar Live.
Mashabiki wa Ali Kiba wakishow love.
Ali Kiba na mdogo wake Abdul Kiba wakizidi kuwapagawisha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live.
Ali Kiba akizidi kuitawala steji la kupanda na kushuka la Dar Live.
Baada ya Amber Rose Kutoboa ya Moyoni, Kumbe Wolper Naye afumuka

Baada ya Amber Rose Kutoboa ya Moyoni, Kumbe Wolper Naye afumuka


Baada ya Amber Rose Kutoboa ya Moyoni, Kumbe Wolper Naye Yalishamkuta!!
Mara baada ya hapo jana mwanadada Amber Rose kutoboa ya moyoni na kueleza  kuwa  Wiz Khalifa ndio mwanaume pekee ambae anampa furaha na hatojali watu wanasema nini.