DIAMOND:WEMA HATUKUENDANA TABIA ILIKUWA LAZIMA TUACHANE

Diamond: Ilikua ni lazima kuachana na Wema.STAA Bongo flava kwa sasa Naseeb Abdul Jumaa “Diamond plutnums”, amefunguka kuwa ilibidi aachane na Wema Sepetu ili maisha mengine yaendelee.
 
Kupitia mitikisiko ya pwani, Diamond amedai mara kadhaa alitumia nguvu nyingi kujenga mahusiano yake bila mafanikio, kwa kuwa yeye na Wema “Madame” hawakuendana tabia.
“Nafikiri hatukuendana tabia kwa kuwa nilifanya kila niwezalo, tulikubaliana kwa pamoja na ikafika hatua ikawa ni lazima tuachane tu” alifunguka Chibu “diamond”.

Kwenye line nyingine Plutnumz alithibithibitisha rasmi ujauzito wa kichuna wake wa sasa Zarrina Hassan “Zarri the boss lady”, na kumpa sifa mob kuwa ni mwanamke wa pekee aliyekubali kupata nae mtoto

“Mabinti wengi niliokua nao, na hata wa hapa mjini kukubali kua na mtoto ni jambo zito sana so nina kila sababu ya kumshukuru sana na nampenda kwa kweli” alimalizia Diamond.