NEW AUDIO:SONGA FT SUSUMAN- JUU KWA JUU/DOWNLOAD

Rapper Songa Ameachia single yake mpya "Juu kwa Juu" aliyomshirikisha Susuman
iliyotengenezwa  na producer Ray Technohama 
BOFYA CHINI KU DOWNLOAD
BOFYA HAPA KUDOWNLOAD
Davido azomewa na wakenya kwa Show fupi simu zake zaporwa!

Davido azomewa na wakenya kwa Show fupi simu zake zaporwa!

 1971476_403424773151654_1766722506_n

 Wakenya wamechukizwa na show fupi ya Davido iliyofanyika Jumamosi hii kwenye viwanja vya Carnivore jijini Nairobi.
Inasemekana kuwa show yake ilidumu kwa takraban dakika 30 tu licha ya kuwa na kiingilio cha shilingi 45,000 za Tanzania. Msanii huyo alilipwa shilingi milioni 146 za Tanzania kutumbuiza kwenye show hiyo.SOMA HAPA ZAIDI ALICHOPOST>>>>>>>
MFAHAMU MTANZANIA WA KWANZA KUSIGN LABEL STUDIO ZA UNIVERSAL MUSIC BAADA YA KUSHINDA SHINDANO LA AIRTELTRACESTAR

MFAHAMU MTANZANIA WA KWANZA KUSIGN LABEL STUDIO ZA UNIVERSAL MUSIC BAADA YA KUSHINDA SHINDANO LA AIRTELTRACESTAR


11078950_1640752309489044_2004175639_n Mayunga akiwa na Akon baada ya kutangazwa mshindi
 Muimbaji wa Tanzania, Mayunga Jumamosi hii alishinda shindano la Airtel Trace Music Star lililoandaliwa kwa ushirikiano wa kituo cha Trace TV, Airtel na muimbaji mwenye asili ya Senegal, Akon.
Fainali za shindano hilo lililohusha nchi takriban 12, zilifanyika jijini Nairobi, Kenya ambapo Akon alikuwa mmoja wa majaji wa shindano.
10249302_1550781318519068_1517746496_n
Kwa ushindi huo, Mayunga amepata deal ya kuwa chini ya label ya Akon, Kon Live na Universal Music Group.
ALI KIBA NA LADY JAY DEE WAME TISHA SANA KWENYE SHOW YAO ILIO FANYIKA M.O.G BAR&RESTAURANT TAZAMA PICHA HAPA

ALI KIBA NA LADY JAY DEE WAME TISHA SANA KWENYE SHOW YAO ILIO FANYIKA M.O.G BAR&RESTAURANT TAZAMA PICHA HAPA

DSC_0035
Mwanamuziki Lady Jay Dee akitoa burudani na Machozi Band Ijumaa ya tarehe 27 mwezi huu ndani ya kiota chake cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge) katika show anazofanya mara moja kwa mwezi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo Ijumaa hiyo alimualika Msanii machachari wa Bongo Flava Ali Kiba kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya kiota hicho.
DSC_0033
DSC_0058
Vijana watanashati wenye vipaji vya aina yake wa Machozi Band wakipiga Back Vocal kumpa sapoti Lady Jay Dee a.k.a Komando Binti Machozi. Kutoka kushoto ni Faraja, Omirady pamoja na Chiqitita.
 
DSC_0089
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Machozi Band wakimtunza manoti Lady Jay Dee.
DSC_0083
DSC_0078
DSC_0046
Umati wa mashabiki wa Machozi Band wakipata burudani kutoka kwa band hiyo inayoongozwa na Lady Jay Dee.
DSC_0048
DSC_0065
DSC_0066
DSC_0204
Msanii nyota nchini, Ali Kiba akitoa burudani ya aina yake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant baada ya kutikia mualiko wa msanii mwezake Lady Jay Dee na kufanya Live Music bila kutumia CD na kuwafanya mashabiki kupagawa zaidi.
DSC_0217
Ali Kiba akiendelea kuwaburudisha mashabiki wake Machozi Band.
DSC_0219
Warembo walipagawajem sasa.
DSC_0248
Twende kazi hapo sasa.
DSC_0253
Mrembo akijinafasi kwa Ali Kiba.
DSC_0275
#ChekechaCheketua.......Wadada wakichizika na mauno ya Ali Kiba na style yake mpya.
DSC_0283
Mwanadada hakukubali kabisa na kuamua kupanda jukwaani kulipiza mauno ya Ali Kiba.
DSC_0284
Picha inajieleza jinsi Ali Kiba alivyokonga nyoyo za mashabiki wake.
DSC_0296
Lady Jay Dee: Nimemkuta analia, kajilaza, sababu amechoka.....Mengi amevumilia, yalomkwaza, anataka kuondoka....ana siku ya pili sasa, hajarudi nyumbani kulala,...namuonea huruma sana, haya....mapenzi hayana maana
Lady Jay Dee: who the single girl.....who the single boy, Ali Kiba: i am a single boy.......Ali Kiba: who the single girl, .......Lady Jay Dee: i am a single girl.......Lady Jay Dee: who the single boy, Lady Jay Dee na Ali Kiba:....mi na we single boy.
DSC_0300
Tumefunika mbaya mtu wangu....ndio ishara waliyokuwa wakipeana Ali Kiba na Lady Jay Dee.
DSC_0281
DSC_0256
DSC_0010
Binti mrembo binti kwenye kipaji Faraja wa Machozi Band akiwapa raha mashabiki wa Band hiyo Ijumaa ya mwisho wa mwezi huu ndani kiota cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge).
DSC_0142
Mkali wa Reggae na Dance Hall nchini Double D akiwarusha mashabiki wake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.
DSC_0158
Mkali wa Reggae na Dance Hall nchini Double D katika hisia kali za kuwapa raha mashabiki wake.
DSC_0144
Vijana wakijiachia vilivyo baada ya Reggae za Double D kuwakolea ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.
DSC_0170
Omirady wa Machozi Band akitoa burudani kwa mashabiki wa Band hiyo katika show inayopigwa mara moja kwa mwezi na kuwateka mashabiki wengi ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.
DSC_0015
Msanii Chiqitita wa Machozi Band akitoa burudani kwa mashabiki wa band hiyo (hawapo pichani).
DSC_0059
Mashabiki wa machozi band wakipata Ukodak.
DSC_0193
Sehemu ya umati wa mashabiki wa Live Band uliofurika Ijumaa ya mwisho wa mwezi huu ndani ya M.O.G Bar & Restaurant kushuhudia show ya wakali wa muziki nchini Lady Jay Dee na Ali Kiba.
DSC_0001
Hawa jamaa ndio wanaohakikisha Lady Jay Dee anakuwa salama siku zote.
Soma Chanzo cha Kifo cha BOSS wa Tip Top Connection ABDUL BONGE na Picha za Waliohudhuria Msibani Leo Ziko Hapa

Soma Chanzo cha Kifo cha BOSS wa Tip Top Connection ABDUL BONGE na Picha za Waliohudhuria Msibani Leo Ziko Hapa


Umati wa vijana ukiwa hauamini kutokea kwa kifo cha Abdul Bonge.
Meneja wa TMK Wanaume Family, Yamoto Band na Diamond, Said Fella akiwaeleza kinachoendelea baadhi ya mastaa waliofika msibani hapo.
Msanii wa filamu za Kibongo, Baba Haji, akiwaelekeza wenzake ulipo msiba.
Mdogo wa marehemu Abdul Bonge, Bab Tale akihojiwa na Mwandishi Mwandamizi na Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Global Publishers, Richard Bukos.
Fella akiwaeleza jambo vijana wake.
Waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni msibani hapo.
Mdogo wa marehemu, Habib Uledi (kushoto) akimueleza jambo msanii wa filamu za Kibongo, William Mtitu.
Wasanii wa filamu za Kibongo, Baba Haji na Riyama Ally wakisalimiana kwa kimtindo.
Mchekeshaji Kitale a.k.a ‘Mkude Simba’ akiingia msibani huku akifuatiwa na mchekeshaji mwenzake, Stan Bakora.
Wasanii wa filamu za Kibongo wakisalimiana.
Mdogo wa marehemu aitwaye Idd ambaye alikuwa ndiye wa kwanza kuitwa baada ya kaka yake kuanguka.
Kitale na Baba Haji wakifurahia jambo baada ya kukutana.
KIFO cha mdau wa muziki nchini ambaye ni mwanzilishi na meneja wa kundi la Tip Top Connection, Abdul  Shaban Taletale, kilichotokea Magomeni-Kagera jijini Dar es Salaam, jana jioni kimeendelea kuzua utata kufuatia mtuhumiwa wa mauaji mtu aliyetajwa kwa jina la Nassoro Idd kuingia mitini.
Akizungumza na mtandao huu, Meneja wa Kundi la Tip Top Connection na mdogo wa marehemu, Hamisi Shaban ‘Bab Tale’, alisema siku ya tukio Abdul Bonge akiwa maskani ya Tip Top Connection iliyopo Magomeni-Kagera alifuatwa na kijana mmoja na kuambiwa rafiki yake aitwaye Nassoro Idd alikuwa akipigana na mkewe hivyo aliagizwa na mama yake Nassoro akamwite ili awasuluhishe.
Muda mfupi baada ya kwenda kwenye ugomvi huo zilirudi taarifa kuwa Abdul Bonge ameanguka na kupoteza fahamu. 
Bab Tale alisema walimpeleka Hospitali ya Saint Monica iliyopo Manzese-Darajani lakini waliambiwa tayari ndugu yao alikuwa amepoteza maisha. Kufuatia tukio hilo Nassoro ametorokea kusikojulikana lakini mkewe anashikiliwa na jeshi la polisi.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa muda wowote kwenda Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro baada ya polisi kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo na kuwakabidhi mwili huo.