Lady jaydee ft dabo Forever teaser

Lady jaydee ft dabo Forever teaser

Sikiliza hapa wimbo mpya wa DITTO “HERI YA CHRISTMAS”

Sikiliza hapa wimbo mpya wa DITTO “HERI YA CHRISTMAS”


artist_1183c0d4e0d39717a570a2ef73fd68a8d90
Msimu wa Christmas ndiyo unatufikia sasa na wimbo wa kwanza wa Christmas ndiyo huu hapa kutoka kwa Ditto. Ditto ambaye ameandika nyimbo nyingi ambazo ni hits kubwa katika muziki wa Tanzania pia ni mwimbaji na mwalimu wa muziki Tanzania House of Talent.
Huu ni wimbo unaofuata baada ya “Ntampata wapi?” ya Diamond Platnumz

Huu ni wimbo unaofuata baada ya “Ntampata wapi?” ya Diamond Platnumz




diamond platnumz 
Chibu Dangote “Diamond Platnumz” ameongelea kuhusu maamuzi ya kutoa wimbo huu wa “Ntampata Wapi?” na wimbo wake mwengine ambao bado hajauweka wazi jina lake. Diamond ameeleza haya akiwa anajadiliana na Bab Tale mmoja kati ya watu wanao M Manage.

“Kama wanaitaka na imekaa tu ndani haina kazi, wape tu basi Mashabiki zako…. kisha kabla ya mwaka kuisha Watolee hiyo unayoitaka wewe….”
Nikamwambia – “sawa Boss Tale”

JOSLIN AJA NA UJIO MPYA



 
NA SYLVESTER DAVID
MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka katika kundi la ‘Wakali kwanza’,  Joslin Mchalla maarufu kama Joslin anatarajia kutambulisha kibao chake kipya hivi karibuni.

Akizungumza na MUZIKI BEGANI alisema amefanya kibao kizuri kitakachokonga nafsi za mashabiki wake.
NEWS: Kumbe kuwa KIMYA kwa MABESTE (@MabesteBudaa) sababu zake zilikuwa ni hizi…

NEWS: Kumbe kuwa KIMYA kwa MABESTE (@MabesteBudaa) sababu zake zilikuwa ni hizi…



w

Msanii Mabeste Venance aka Mabeste kwenye ukurasa wake wa Facebook ameshare kitu kizuri kwa mashabiki wake na kuwaeleza sababu za yeye kuwa kimya kwa muda wa miezi kazaa.. Mabeste aliandika status hii..

EXCLUSIVE NEWS I am back people!!! My New Audio Actually Imeisha Iko Ready Tunaangalia Tuu Hali Ya Hewa Soon Nitaachia! Sorry Watu Wangu!! Kwa Ukimya Ilikua Time Ya Kendrick Ku Enjoy Na Dad After He Was Born Now Nimerudi Kazini!! Thanks Watu Wangu Kwa Uvumilivu!!

BAADA YA KUTAMBA NA 'RUN DSM', KITWANA ARUDI NA SIFA 10 ZA MREMBO

MSANII chipikizi anayekuja kwa kasi katika muziki wa Hip Hop nchini, Kitwana Ramadhani ‘Kitwana’ amesema anatarajia kutambulisha video ya kibao chake kipya kijulikanach kama ‘Sifa kumi za mrembo’. mwanzoni mwa mwezi Desemba .
Akizungumza na MUZIKI BEGANI alisema video hii ni nzuri na imebeba ujumbe mzuri ambao naamini mashabiki wataupenda.
“Natarajia kutambulisha video ya wimbo wangu mpya ambayo ni video nzuri inayozungumzia sifa za mwanamke ambaye mtu yoyote anamtaka ana amaweza kumchagua kwa ajili ya ndoa”.Alisema Kitwana.
Kitwana ambaye aliwahi kutamba na kibao kilichojulikana kama ‘Run Dsm’ ambacho kilipigwa katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Kitwana aliwataka mashabiki wake waisapoti video ya wimbo huo na kuwasihi wazidi kusubiri mambo mengi kutoka kwake.



PROFIT:PRODUCER DUNGA AMENIJENGA KIMUZIKI



NA SYLVESTER DAVID
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya nchini Profit Ramadhani maarufu kama Profit amemtaja mwandaaji mkongwe wa muziki nchini,Ambrose Dunga, ‘Dunga’ kuwa ndiye aliye mfanya ajulikane kwa mashabiki wake.

Akizungumza na MUZIKI BEGANI alisema kufanya kazi na mwandaaji huyo kumechangia afanye kazi nzuri zinazopendwa na mashabiki wa muziki nchini.
“Dunga ni mwandaaji anaujua vizuri mziki na maisha halisi ya wasanii nchini,nimefanya naye kazi tatu nzuri zinazolenga soko na wapenzi wa muziki nchini”.Alisema Profit.

Awali Profit aliwahi kutamba na kibao cha ‘Hawana tena ubinadamu’ alichomshirikisha msanii Sunday Mjeda maarufu kama ‘Linex’ kilichofanyika katika studo za Sharobaro Record Magomeni jijini Dar es salaam.

Profit aliongeza kuwa akiwa chini ya mwandaaji Dunga alifanya vibao vitatu kikiwemo ‘All about Profit’ alicho mshirikisha mwandaaji huyo.

Vilevile aliongeza kuwasihi mashabiki wake wakae tayari kuipokea video ya wimbo wake mpya aliomshirikisha msanii Yard ijulikanayo kama ‘Sirud nyuma’.
SHOWDAR:'MKURUMBATI ITANITOA KIMUZIKI'

SHOWDAR:'MKURUMBATI ITANITOA KIMUZIKI'



NA SYLVESTER DAVID
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya nchini Meck Simon maarufi kama Showdar amesema kuwa wimbo wake wa ‘Mkurumbati’ utamtambulisha vizuri kwa mashabiki wake.

Akizungumza na MUZIKI BEGANI alisema amefanya wimbo mzuri unaochezeka ambao ataamini utapendwa zaidi na mashabiki wake.

“Nimefanya vizuri katika wimbo wangu huu ikiwemo kuonesha vilivyo kipaji changu, ambao ntautambulisha hivi karibuni katika vyombo mbalimbali vya habari nchini”.Alisema Showdar.

Showdar ambaye aliwahi kutola na kibao kijulikanacho kama ‘kosa si kosa’, ambacho hakimtambulisha vizuri kutokana na ugeni katika tasnia ya muziki nchini.

Showdar ambaye yuko chini ya mwaandaaji chipukizi mwenye kipaji kikubwa cha muziki nchini ajulikanaye kama ‘Mkongo Shentee’ kati.ka studio za African Music Lab.

Pia aliwataka mashabiki wake kusubiri kazi nyingi kutoka kwake na na kuisapoti  studio yaa African Music Lab kwa ujumla.

MISS HAPPINESS WATIMANYWA KUKWEA PIPA KESHO



 
NA SYLVESTER DAVID
MSHINDI wa taji la Redd's Miss Tanzania mwaka 2013,Happiness Watimanywa, leo anaondoka nchini kwenda Mjini London Uingereza kwa ajili ya kushiriki Miss World.

Shindano hilo litafanyika desemba 14,mwaka huu kutokana na kubalishwa utaratibu wa shindano ambao lilikuwa likifanyika ndani ya mwaka baada ya kushinda na kubadilishwa kisha kufanyika mwaka mmoja baada ya kushinda taji la nchi kama ilivyo sasa. 
Miss Happiness akiwa na washindi wenzake akipochukua taji

AkizungumzaMUZIKI BEGANI alisema amefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kushiki vizuri taji hilo.

"Nimepata sapoti ya kutosha kwa ajili ya safari hiyo kutoka taasisi na makampuni mbalimbali ikiwemo Bodi ya utalii nchini na wanamitindo mbalimbali nchini".Alisema Watimanywa.

Watimanywa alisema kupitia shindano hilo atapata nafasi ya kuitangaza Tanzania na vivutio vilivyopo nchini kutokana na kutengeneza vipindi mbalimbali vya kuonesha vivutio mbalimbali  nchini walivyotengeneza kupitia bodi ya utalii nchini.


Vilevile aliongeza kuwa namna mbalimbali ya kuwapigia kura kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo facebook/miss world tanzania,Twitter@watimanywa na instagram@hapinesswatimanywa.