UJIO WA NGOMA MPYA YA KALA JELEMAYA-USIKATE TAMAA

http://s1.hulkshare.com/song_images/original/4/b/1/4b17afb7fda54d55d289ce1ae1507925.jpg?dd=1388552400
NA SYLVESTER DAVID
MSANII nguli wa muziki wa Hip Hop nchini, Kala Jelemiah maarufu kama Kalla Jelemaya anatarajia kuachia wimbo wake mpya ujulikanao kama ‘usikate tamaa’.

Akizungumza na MUZIKI BEGANI alisema wimbo huo atauachia rasmi katika vyombo mbalimbali vya habari nchini Novemba 23 mwaka huu.

“Wimbo huu umebeba dhamira ya kuwafariji watu mbalimbali wenye matatizo na kuwapa moyo na nguvu za kusonga mbele”.Kalla Jelemaya alisema.

Kalla ambaye pia ni balozi wa kampuni ya Pepsi nchini  na aliwahi kutamba na nyimbo zake kibao zikiwemo ,Wimbo wa Taifa, Waambieni na  Dear God.

Vilevile aliongeza kuwa wimbo huo utatambulishwa novemba 23 ambao utatambulishwa pamoja na video ya wimbo huo.
Pia aliwataka mashabiki wake wakae tayari kwa kazi nyingi na nzuri kutoka kwake.