SHOWDAR:'MKURUMBATI ITANITOA KIMUZIKI'



NA SYLVESTER DAVID
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya nchini Meck Simon maarufi kama Showdar amesema kuwa wimbo wake wa ‘Mkurumbati’ utamtambulisha vizuri kwa mashabiki wake.

Akizungumza na MUZIKI BEGANI alisema amefanya wimbo mzuri unaochezeka ambao ataamini utapendwa zaidi na mashabiki wake.

“Nimefanya vizuri katika wimbo wangu huu ikiwemo kuonesha vilivyo kipaji changu, ambao ntautambulisha hivi karibuni katika vyombo mbalimbali vya habari nchini”.Alisema Showdar.

Showdar ambaye aliwahi kutola na kibao kijulikanacho kama ‘kosa si kosa’, ambacho hakimtambulisha vizuri kutokana na ugeni katika tasnia ya muziki nchini.

Showdar ambaye yuko chini ya mwaandaaji chipukizi mwenye kipaji kikubwa cha muziki nchini ajulikanaye kama ‘Mkongo Shentee’ kati.ka studio za African Music Lab.

Pia aliwataka mashabiki wake kusubiri kazi nyingi kutoka kwake na na kuisapoti  studio yaa African Music Lab kwa ujumla.