PROFIT:PRODUCER DUNGA AMENIJENGA KIMUZIKI



NA SYLVESTER DAVID
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya nchini Profit Ramadhani maarufu kama Profit amemtaja mwandaaji mkongwe wa muziki nchini,Ambrose Dunga, ‘Dunga’ kuwa ndiye aliye mfanya ajulikane kwa mashabiki wake.

Akizungumza na MUZIKI BEGANI alisema kufanya kazi na mwandaaji huyo kumechangia afanye kazi nzuri zinazopendwa na mashabiki wa muziki nchini.
“Dunga ni mwandaaji anaujua vizuri mziki na maisha halisi ya wasanii nchini,nimefanya naye kazi tatu nzuri zinazolenga soko na wapenzi wa muziki nchini”.Alisema Profit.

Awali Profit aliwahi kutamba na kibao cha ‘Hawana tena ubinadamu’ alichomshirikisha msanii Sunday Mjeda maarufu kama ‘Linex’ kilichofanyika katika studo za Sharobaro Record Magomeni jijini Dar es salaam.

Profit aliongeza kuwa akiwa chini ya mwandaaji Dunga alifanya vibao vitatu kikiwemo ‘All about Profit’ alicho mshirikisha mwandaaji huyo.

Vilevile aliongeza kuwasihi mashabiki wake wakae tayari kuipokea video ya wimbo wake mpya aliomshirikisha msanii Yard ijulikanayo kama ‘Sirud nyuma’.