Producer Tudd Thomas avamiwa na vibaka

Producer Tudd Thomas avamiwa na vibaka

http://s0.hulkshare.com/avatar_images/original/7/e/c/7ec3347da4d0db84f302c270b1779b45.jpg?dd=1388552400

Mtayarishaji wa muziki nchini, Tudd Thomas amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikika kuwa ni vibaka maeneo ya Mlimani City, jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye ukurasa wa @Cloudsfmtz Instagram, Mtayarishaji huyo aliyetengeneza hits za mastaa mbalimbali akiwemo Diamond ‘Mdogo Mdogo’, amelazwa hospitali ya Muhimbili katika kitengo cha MOI.

Tudd
Haya ni maelezo ya BASATA kuhusiana na kumfungia Shilole

Haya ni maelezo ya BASATA kuhusiana na kumfungia Shilole

 http://www.gongamx.com/wp-content/uploads/2014/03/63b7e38ab0ea11e3a7630e29514d93ff_8.jpg

Baraza la Sanaa la taifa, BASATA, limemfungia Shilole kutojihusisha na masuala ya muziki ndani na nje ya Tanzania kwa mwaka mmoja.


BASATA limempa barua Shilole jana yenye taarifa za kufungiwa kwake. 

Adhabu hiyo imetolewa kufuatia tukio la msanii huyo kupigwa picha za aibu wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji miezi kadhaa iliyopita.

Hii ni taarifa rasmi ya BASATA:
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini limemfungia msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Zuena Mohamed kwa jina la kisanii Shilole kufanya shughuli za sanaa nchini kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe 24/07/2015 hadi tarehe 24/07/2016.

Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 09/05/2015 akiwa katika onyesho lake la Muziki nchini Ubelgiji alikiuka maadili ya kazi ya sanaa mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania na hivyo akadhalilisha utu wake na jamii ya Kitanzania kimaadili.

Pia itakumbukwa kwamba mnamo mwezi Oktoba, 2013 BASATA ilimuonya na akakiri kwa kuomba msamaha kwa tabia yake ya kucheza bila kuzingatia utu na maadili awapo jukwaani.

BASATA ilimpa nafasi ya kutoa maelezo yake kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chake cha kudhalilisha maadili, utu na sanaa ya Tanzania lakini akakaidi kutoa maelezo. Hivyo basi BASATA imejiridhisha kwamba alikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onesho lake la huko Ubelgiji makusudi na amekiuka Sheria, Kanuni na Taratibu za uendeshaji wa Sanaa.

Hivyo basi kutokana na ukiukwaji huo wa sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini, Baraza la Sanaa la Taifa chini ya Kanuni ya 30(1)(d) ya G.N 322 ya 2005 limemsimamisha kujishughulisha na kazi za Sanaa nchini kwa muda wa Mwaka Mmoja tokea tarehe 24/07/2015.

Hivyo haruhusiwi kufanya au kushiriki kwa namna yoyote ile shughuli yoyote ya onesho la sanaa nchini au nje ya nchi. Iwapo atafanya kinyume cha hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi ikiwa ni pamoja na yeyote yule utakaye shirikiana naye.

Ni matumaini ya Baraza la Sanaa la Taifa kwamba wasanii na waandaaji wa shughuli za sanaa wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

Shilole aliwahi kusema kuwa hata yeye hakupenda kile kilichotokea jukwaani wakati akitumbuiza nchini humo kwa sababu ilikuwa bahati mbaya na hakudhamiria kukaa uchi kama wengi wanavyosema.
Shishi ambaye ni mama wa watoto wawili alisema kuwa nguo mpya aliyoivaa siku hiyo ndio ilimponza kwasababu hakuwa ameifanyia majaribio ya kutumbuiza akiwa ameivaa.

“Kiukweli kwasababu hili jambo limetokea inatakiwa nguo ninapoinunua niwe naifanyia training kwanza kabla ya kwenda jukwaani, kwahiyo kwasababu ile nguo ilikuwa mpya kwangu na sikuweza kuijua vizuri […] yaani hii nguo nimeikuta huku huku, nguo imekuja kunitokea bahati mbaya wakati niko kwenye performance, ilitatuka wakati niko kwenye motion,” Shishi aliiambia Clouds FM.
Aliongeza kuwa alisikitishwa na mtu aliyempiga picha hizo na kuamua kuzisambaza mtandaoni bila kujua kuwa itamuumiza yeye kama mwanamke.

“Nasisitiza tena sikudhamiria na wala sikupenda hiyo kitu itokee, ila nasikitika kwamba kama mimi mwanamke yule mtu aliyenipiga picha na kudhamiria kuziweka kwenye mitandao alikuwa na maana gani, hakufikiria mimi nitaunmia kiasi gani au mashabiki wangu wataumia kiasi gani? Ni mtu mbaya mwenye roho mbaya sijui nimuiteje huyo mtu aliyefanya hivyo, sio mtu mzuri.”

Unachukuliaje adhabu hiyo? Ni halali ama Shilole ameonewa?
 Omondi kuzivunja mbavu za wakazi wa Dar Jumamosi hii

Omondi kuzivunja mbavu za wakazi wa Dar Jumamosi hii

11385578_105229463160025_615348516_n

Mchekeshaji maarufu Eric Omondi na bendi ya muziki ya SARABI kutoka Kenya wataungana na wanamuziki wa Tanzania Grace Matata na Leo Mkanyia na bendi yake ya Swahili Blues kukonga nyonyo za mashabiki wa muziki na vichekesho jijini Dar es Salaam wakati wa onyesho la muziki Jumamosi wiki hii.

Onyesho hilo ambalo limeandaliwa na CDEA:“Culture and Development East Africa” kwa kushirikiana na Nafasi Art Space litafanyika jumamosi ya tarehe moja mwezi wa nane mwaka huu, kuanzia saa moja jioni mpaka asubuhi katika ukumbi wa Nafasi Art Space-Mikocheni.

Mratibu wa onyesho hilo Naamala Samson alisema kuwa mbali na onyesho hilo pia kutakuwa na burudani kemkem kutoka kwa maDJ wa Santuri Safari kutoka Kenya na Uganda.

“Wanamuziki wote wamefanya mazoezi ya kutosha na wamejiandaa kikamilifu kwa onyesho hili la kihistoria, ni siku hiyo watanzania watapata fursa ya kuonja ladha ya muziki wa Afrika Mashariki wenye vionjo vya nyumbani na kupata vichekesho vya mwaka kutoka kwa Omondi,” alisema Naamala.

Bendi ya Sarabi ni miongoni mwa bendi kubwa na zinazofanya vizuri nchini Kenya na kuwepo kwake kwenye tamasha hili kutanogesha mambo na kutoa burudani ya kutosha kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani.
Bila P-Funk, Marco Chali, Pancho nisingeiva kama producer โ€“ Dully Sykes

Bila P-Funk, Marco Chali, Pancho nisingeiva kama producer – Dully Sykes

 Dully
Dully Sykes amemtaja producer wa Bongo Records, P-Funk Majani kuwa ni miongoni mwa watu waliomfundisha mambo mengi kuhusiana na utayarishaji wa nyimbo.

Dully aliwahi kumiliki studio iitwayo Dhahabu Records kabla ya kuanzisha nyingine 4.12 iliyopo hadi sasa ambapo yeye mwenyewe ndiye producer.
“Namshukuru sana P-Funk maana yeye ndo kati ya maproducer walionisaidia na kunifundisha hata kugonga kick na snare,” Dully aliiambia E-News ya EATV.
“Alikuwa ananiambia kuwa kiCi inatakiwa KUWA katika level ipi ili muziki usikike vizuri, yaani namshukuru amenifundisha vingi. Na mtu kama Marco Chali alikuwa sio mchoyo kunipa vitu. Namshukuru pia Pancho ni mdogo wangu nimemlea mwenyewe na Producer Mbezi, hawa ni wadogo zangu wamenisaidia sana.”
Exclusively video mpya ya Mayunga, mshindi wa Airtel Trace Music Star kurushwa Trace Urban Ijumaa hii

Exclusively video mpya ya Mayunga, mshindi wa Airtel Trace Music Star kurushwa Trace Urban Ijumaa hii

 

Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star, Mtanzania Mayunga Malimi anategemea kuachia video yake mpya ‘Nice Couple’ ambayo itaoneshwa kwa mara ya kwanza na kituo cha Trace Urban cha Ufaransa Ijumaa hii July 31.


Mayunga ambaye alienda Afrika Kusini kushoot video hiyo, amewataarifu mashabiki wake Kupitia ukurasa wake wa Intagram.



“Aya wadau wangu jumlisha na manice couples watoto kwa wa kubwa wimbo wenu una dondoka kesho kwenye kituo cha trace tutupie macho ili kuweza kuona kazi ya kijana wenu hop mtafurahia asanteni na nawapenda sana.”– Mayunga

Kupitia shindano la Airtel Trace Music Star ililofanyika mapema mwaka huu, Mayunga alishinda mkataba wa kurekodi muziki na label ya Universal Music wenye thamani ya $500,000.
pata nafasi ya kuwapigia kura wakongwe hawa wa Bongo Movies

pata nafasi ya kuwapigia kura wakongwe hawa wa Bongo Movies

Wapigie Kura Wakongwe Hawa wa Bongo Movies, Unayemkubali

  • Wapigie Kura Wakongwe Hawa wa Bongo Movies, Unayemkubali 1
  • Wapigie Kura Wakongwe Hawa wa Bongo Movies, Unayemkubali 2
  • Wapigie Kura Wakongwe Hawa wa Bongo Movies, Unayemkubali 3
  • Wapigie Kura Wakongwe Hawa wa Bongo Movies, Unayemkubali 4
  • Wapigie Kura Wakongwe Hawa wa Bongo Movies, Unayemkubali 5
  • Wapigie Kura Wakongwe Hawa wa Bongo Movies, Unayemkubali 6
  • Wapigie Kura Wakongwe Hawa wa Bongo Movies, Unayemkubali 7
Kutangaza hapa piga : 0715577805
KATIKA kinyang’anyiro cha tuzo za filamu Tanzania (TAFA) zitakazotolewa mwaka huu kuna mchuano mkali kwa kuwakutanisha wasanii wenye uwezo wa juu kipengele hiki cha Time Life achievement unakutana na vichwa kama vile Thecla Mjatha, Farida Sabu, Susan Lewis ‘Natasha’, Hashim Kambi, Ahmed Olotu.
Wengine ni Chuma Seleman, Hidaya Njaidi, na msanii ambaye aliwahi kushinda kama mshindi Bora wa Karne huko Ujerumani Bakary Mbelemba ‘Mzee Jangala’ msanii jembe kwa kuwawezesha kushinda wasanii hawa andika namba yake iliyopo katika picha yake kwenda 15522.
Kwa kufanya hivyo utakuwa umemsaidia msanii wako kushinda na kumtia moyo kwa mchango wake alioutoa kwa jamii ya Tanzania mpigie msanii umpendae kuibuka kinara kutoka Tanzania film awards TAFA.

PITIA MAGAZETI YA LEO IPO HABARI YA MADEREVA KISITISHA MGOMO KWA KUIPA SERIKALI MASHARTI,YANGA KUSHEREKEA UBINGWA NA YANGA NA VAN PERSIE APATA LAKUNGEA>>>>>>SHUKA NAYO




NEW AUDIO:Baraka Da Prince - Baraka Da Prince Ft Linah - Siachani Nawe (Remix):

GARI LA KANUMBA LAGOMA KUTOKA SOKONI

GARI LA KANUMBA LAGOMA KUTOKA SOKONI


Gari la Kanumba Lashindwa Kuuzika Sokoni
Ikiwa ni miaka mitatu sasa imepita tangu aliekuwa staa wa Bongo  Movies, marehemu Steven Kanumba, inadaiwa kuwa gari alilokuwa akilitembelea aina ya Toyota Lexus lenye namba za usajili T750 AER limezidi kudoda sokoni.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti la Risasi kimepenyeza habari kuwa gari hilo lililonunuliwa na marehemu kwa shilingi milioni 78, linapatikana maeneo ya Msasani, jijini Dar kwenye jengo la mikopo ambapo linauzwa kwa bei chee ya shilingi milioni 18 hadi 14.
“Nilikuwa nikijipitia kukagua magari lakini ghafla nikakutana na gari la Kanumba. Sikuamini mpaka pale nilipoingia na kulipiga picha kisha nikaambiwa na thamani yake,” kilisema chanzo.Chanzo kiliendelea kutiririka kuwa huenda kuna mkopo ulichukuliwa na kuacha dokumenti zote za gari hiyo na iliposhindikana kulipwa gari hiyo ikapigwa mnada.
“Sidhani kama gari kali kama ile ipigwe bei ya milioni 18 tu, lazima kutakuwa na mkopo ambao haujamalizwa ndiyo maana limepigwa kiasi hicho cha pesa ili kukamilisha.”Awali ilisemekana kuwa gari hilo lilikabidhiwa kwa msanii wa filamu Bongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ ili alinunue kwa gharama ya shilingi milioni 40 lakini kwa kuwa liligundulika na matatizo mengi akawa tayari kutoa shilingi milioni 25 ambapo pia ilishindikana na kurudishwa kwa familia ya Kanumba.
Gazeti hilo lilimtafuta mama Kanumba, Flora Mtegoa ili kujua anazungumziaje gari hilo kudoda sokoni, alijibu:“Mimi sijui chochote kuhusu hilo gari naona mnazidi kuniumiza tu hapa naumwa, hata kama nimeuza au limefanywaje jamani maswali mengine yanaumiza hebu niacheni maana sijui kinachoendelea kuhusu hilo gari,” alisema Mama Kanumba.