IFAHAMU HISTORIA YA MSANII VANNESA MDEE


Vanessa Hau Mdee maarufu kama Vee Money alizaliwa juni 7,1988 mjini Arusha Tanzania,ni msanii wa muziki,mwandishi wa nyimbo na mjasiriamali vile vile mtangazaji wa tv na redio.
  Mdee anafahamika kama mwanamke wa kwanza kutoka nchini Tanzania kutanga kituo maarufu cha luninga MTV Vj kuanzia mwaka 2007 na baadaye kutangaza katika shindano la Epic Bongo Star Search na kipindi cha dume katika channel ya ITV .
mwaka 2012 Alijiunga na kundi la B’Hits Na kushirikishwa na Ay katika wimbo ujulikanao kama pia kushirikishwa na wake na msanii OMMY DIMPOZ, katika wimbo ujulikanao kama Me and
akiwa Mtv Mwaka 2008, akiwa balozi wa Alive Foundation moyo wake aliweza kutembelea Uwanja wa fisi na Balozi Kelly Rowland. Mdee pia alijiunga Malaria No More Kampeni, kampeni yenye lengo la kutokomeza malaria.
mwaka 2009 Mdee alitangaza katika maonesho ya Sauti Za Busara International Music Festival,
pia mwaka 2011 alikuwa mtangazaji wa kituo cha radio nchini kijulikanacho kama choice fm na kufanya iterview na wasanii kibao wakiwemo
K'Naan, Kelly Rowland, Mac Miller, Rick Ross, Ludacris, Miguel, Donald, Naazizi, Xtatic, Stella Mwangi, Camp Mulla, Tay Grin, Teargas, Dr. Sid and many more African and international acts.


Vilevile aliwahi kupata tunzo na kushiriki katika kazi na matangazo mbalimbali yakiwemo ya Music Awards, Airtel, Coke Studio, Crown Paints, Music Tours mwaka 2014 na kufanya nyimbo kibao ikiwemo ‘Siri’ ,’Hawajui’, ‘Closer’