HIKI NDICHO Walichokiamua Orijino Komedi kuhusu aliyezusha kifo cha Vengu.. kuna movie mpya ya Sharo milionea?





KO 1

Baada ya uvumi kusambaa kuwa mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi  Vengu amefariki na baadae kaka yake alikanusha uvumi huo, kiongozi wa kundi hilo Sekioni David amesema wamepata usumbufu mkubwa juu ya uvumi huo na wao kama kundi wameamua kuchukua hatua zaidi  ili kukomesha tabia hiyo kwa kuwa sio mara ya kwanza, wamepata ushauri kutoka TCRA ambao wamewashauri kuchukua hatua ili kuweza kujua chanzo cha uvumi huo na kuchukua hatua zaidi kwa wahusika  na muda sio mrefu mhusika atajulikana

Kuhusu Afya ya Vengu amesema ni mzima ila kutokana na ushauri wa daktari anatakiwa awe kwenye utulivu ambao unamfanya awe nje ya kundi lakini yeye bado ni mfanyakazi na anaendelea kulipwa kama kawaida.
kitaleMsanii wa vichekesho Kitale amezungumzia movie ambayo alikuwa amefanya na marehemu Sharo milionea lakini haikuweza kutoka baada ya kutokea kifo chake, kazi waliyoifanya kwa lengo la kuleta mabadiliko na iwe mfano movie  iliyokuwa itoke Desemba 2012,  lakini  baada ya kuona hakuna mabadiliko kama walivyotegemea ameamua kuitoa ili watu wajifunze ambapo anategemea kuitoa mwezi ujao.

Ilikusikiliza story zote bonyeza play hapa chini…