Wasanii WAGOMEA Kikao Cha Tuzo Za KTMA 2015

wakati wasanii wa tanzania wakiwa katika harakati za kufikia kilele cha msimu wa  mpya wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 2015, wadau wa sanaa nchini wamelaani kitendo cha baadhi ya wasanii kukacha mwaliko wa kikao cha tathmini ya tuzo hizo.

Katika maandalizi ya tuzo za KTMA kila mwaka, BASATA huwaalika wasanii wa muziki nchini na wadau mbalimbali wa sanaa kuhudhuria tathmini ya tuzo hizo kwa mwaka uliopita kwa malengo ya kutoa maoni juu ya maboresho ya tuzo hizo kwa msimu mpya.
Katika mwaliko wa mwaka huu wasanii wawili tu ndio walihudhuria huku wengine wakikacha kikao hicho kitu ambacho kimewakera sana wadau wa sanaa nchini kwani kila mwaka baada ya tuzo hizo wasanii wamekuwa wakilalamika juu ya utoaji wa tuzo hizo lakini wameshindwa kufika kutoa maoni yao juu ya vitu gani viiboreshwe katika tuzo hizo.
Wasanii wawili waliofika katika tathmini hizo ni Joh Makini na G-Nako kutoka kundi la Weusi wakati mwaliko huo ulihusisha wasanii wengi wakubwa na wanaofanya vizuri katika muziki nchini.
Aidha kitendo cha wasanii kutohudhuria kikao hicho kimewakera sana wadau wa muziki na wasanii wengine akiwepo member wa Weusi, Nikki wa Pili kiasi cha kutoa ujumbe mkali kwa wasanii juu ya tuzo hizo akisema kuwa hatoelewa kama kutakuwa na lawama baada ya tuzo hizo kutolewa kwani wasanii wamekacha kikao cha tathmini ya tuzo hizo hivyo hawatostahili kulaumu kwa lolote.