Exclusively video mpya ya Mayunga, mshindi wa Airtel Trace Music Star kurushwa Trace Urban Ijumaa hii

 

Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star, Mtanzania Mayunga Malimi anategemea kuachia video yake mpya ‘Nice Couple’ ambayo itaoneshwa kwa mara ya kwanza na kituo cha Trace Urban cha Ufaransa Ijumaa hii July 31.


Mayunga ambaye alienda Afrika Kusini kushoot video hiyo, amewataarifu mashabiki wake Kupitia ukurasa wake wa Intagram.



“Aya wadau wangu jumlisha na manice couples watoto kwa wa kubwa wimbo wenu una dondoka kesho kwenye kituo cha trace tutupie macho ili kuweza kuona kazi ya kijana wenu hop mtafurahia asanteni na nawapenda sana.”– Mayunga

Kupitia shindano la Airtel Trace Music Star ililofanyika mapema mwaka huu, Mayunga alishinda mkataba wa kurekodi muziki na label ya Universal Music wenye thamani ya $500,000.

0 Response to "Exclusively video mpya ya Mayunga, mshindi wa Airtel Trace Music Star kurushwa Trace Urban Ijumaa hii "

Chapisha Maoni