MWILI WA AMIGOLAS UMEZIKWA LEO MAKABURI YA KISUTU

Amigolas enzi za uhai wake
NA SYLVESTER DAVID
Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamejitokeza katika mzishi ya aliyekuwa kiongozi na mwimbaji wa bendi ya Ruvu Stars, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ kwenye makaburi ya Kisutu.
Amigolas ambaye alikuwa msanii wa zamani wa bendi ya African Stars ‘ Twanga Pepeta’, alikumbwa na mauti akiwa amelazwa katika hospitali ya ya Taifa ya muhimbili kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
 
Baadhi ya wanachi wakiwemo wasnii waliobeba mwili wa marehemu
Akizungumza na Tanzania Daima mazishini msanii nguli wa muziki wa aliyewahi kuimbia bendi hiyo na sasa anamiliki bendi ya Kalunde, Deo Mwanambilimbi alisema,alipokea kwa masikitiko ma mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha msanii huyo.
“Amigolas alikuwa msanii mwenye uwezo mkubwa na kipenzi cha mshabiki wengi wa muziki wa dansi nchini na ameacha pengo kubwa sana katika tasnia hii”.Alisema Mwanambilimbi.

Pia Ahmed Jan Olomide, aliyekuwa ziarani chini ambaye ni mtoto wa mkongwe wa muziki wa bolingo wa Jamuhuri ya Kidemocrasia ya Kongo, Koffi Olomide alisema ameguswa na sana na msiba wa msanii mwaenzake hali iliyochangia kuhudhuria mazishi hayo.
Naye msanii mwingine wa bendi ya Twanga pepeta maarufu kama Haji Ramadhani pia alisema amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo chake kutokana na nafasi aliyokuwa nayo katika bendi hiyo.


“Nashindwa kuamini kabisa taarifa za kifo kwani Amigolas alikuwa mtu wa mfano kwa wasanii wengi wa muziki nchini ila yote tumuachie mungu kwani ndiye mwenye mamlaka”.Alisema Haji Ramadhani.

Mazishi hayo yalihudhuliwa na wasanii wengi wa muziki na filamu nchini wakiwemo,Steven Nyerere ,Jacob Steven ‘JB’,Visent Kigosi ‘Ray’ Ali Choki,Charls Baba,Haji Ramadhani,Deo Mwanambilimbi na Mtitu.