WADAU TOENI SUPPORT KWA STUDIO ZA AFRICAN MUSIC LAB


NA SYLVESTER DAVID
MWANDAAJI na msanii chipukizi wa muziki wa wa dini nchini kutoka katika studio za African Music Lab, Godfrey Mwakyusa ‘Mkongo Shentee’ amesema anaamini kazi anazofanya na wasanii wanaochipukia zitamtoa kimuziki.

Akizungumza na MUZIKI BEGANI jijini Dar es Salaam alisema amejipanga vizuri katika uandaaji wa muziki mzuri nchini kutokana na uwezo pamoja na vifaa vyenye ubora vya kufanyia kazi alivyonavyo.

Shentee ambaye anathibitisha uwezo wake kwa mashabiki wake kutokana na kuandaa kibao cha masanii Kitwana  ambacho kilifanya vizuri katika vituo vingi vya vya runinga na redio nchini kilichojulikana kama Run Dsm.

“Nimepania kufanya mapinduzi ya muziki nchini ndiyo maana nafanya kazi na wasanii wanaochipukia ambao naamini wataipa heshima African Music Lab na mimi pia”.Alisema Shentee.

Vilevile alieleza kuwa tayari amefanya kazi na wasanii wengi maarufu wakiwemo Dk Karimu,Beka,Edo Gaga,Max Lopez,Habibu k na Show Dar ambao ataamini watamfikisha mbali.
CALL:O715-577805