MISS HAPPINESS WATIMANYWA KUKWEA PIPA KESHO



 
NA SYLVESTER DAVID
MSHINDI wa taji la Redd's Miss Tanzania mwaka 2013,Happiness Watimanywa, leo anaondoka nchini kwenda Mjini London Uingereza kwa ajili ya kushiriki Miss World.

Shindano hilo litafanyika desemba 14,mwaka huu kutokana na kubalishwa utaratibu wa shindano ambao lilikuwa likifanyika ndani ya mwaka baada ya kushinda na kubadilishwa kisha kufanyika mwaka mmoja baada ya kushinda taji la nchi kama ilivyo sasa. 
Miss Happiness akiwa na washindi wenzake akipochukua taji

AkizungumzaMUZIKI BEGANI alisema amefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kushiki vizuri taji hilo.

"Nimepata sapoti ya kutosha kwa ajili ya safari hiyo kutoka taasisi na makampuni mbalimbali ikiwemo Bodi ya utalii nchini na wanamitindo mbalimbali nchini".Alisema Watimanywa.

Watimanywa alisema kupitia shindano hilo atapata nafasi ya kuitangaza Tanzania na vivutio vilivyopo nchini kutokana na kutengeneza vipindi mbalimbali vya kuonesha vivutio mbalimbali  nchini walivyotengeneza kupitia bodi ya utalii nchini.


Vilevile aliongeza kuwa namna mbalimbali ya kuwapigia kura kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo facebook/miss world tanzania,Twitter@watimanywa na instagram@hapinesswatimanywa.