PIZZO TACHEZ PRODUCER MPYA MWENYE MALENGO YA KUTEKA GEMU NCHINI


NA SYLVESTER DAVID
MWANDAAJI chipukizi wa muziki wa kizazi kipya nchini, Linus Agrey maarufu kama Pizzo Tachez amesema amejipanga vizuri kuhakikisha analiteka soko la muziki nchini.

Akizungumza na MUZIKI BEGANI alisema amefanya kazi studio nyingi ambazo anaamini zimemjenga kimuziki.

Pizzo Tachez ambaye kipaji chake ni DJ ukiachana na na uadaaji wa muziki nchini na amepitia studio mbalimbali zikiwemo Ij Record,Beach Record na Black Record zote za jijini Mbeya na kwasasa Bass Station Record ya Ilala jijini Dar es salaam katika hatua za kuboresha muziki na wasanii. 

“Nimejipanga vizuri kuhakikisha nafanya vema kwa mashabiki wangu na kuwapa burudani inayotakiwa kutoka na uwezo wangu wa kufanya kazi nzuri”.Alisema Pizzo Tachez.

Vilevile aliongeza kuwa amefanya kazi na baadhi ya wasanii maarufu akiwemo Hawa na Chibwa.