Migogoro kati ya maproducer na wasanii inashusha muziki nchini.


            Migogoro ni hali ya kutokuwa na maelewano miongoni mwa jamii inawezekana ikawa ya mtu na mtu au jamii na jamii.
            
           Kwa kawaida migogoro katika jamii huwa haizuiliki na inatakiwa kufanya jitihada madhubuti ili kuiepuka.  
Migogoro hiyo ambayo tayari imeingia  katika muziki imejitokeza baina ya wasanii na maproducer wao.
 Kwa hapa nchini migogoro hiyo imeonekana kuwa sababu ya kutafuta umaarufu zaidi kwa msanii au producer.
            Mgogoro kati ya msanii Diamond na Bob Junior ulileta taswira mpya kwa mashabiki wa muziki wao na sharobaro kwa ujumla.

           Wangekaa chini na kumaliza tofauti zao kwa wakati ule tungepokea muziki wa tofauti kutoka kwao.
          Kama ilivyowazi karibu asilimia 75 ya albamu ya kwanza ya Diamond alifanya Producer huyo ambaye ndiye aliyemtoa kimuziki mwenye studio zake magomeni jijini dar es salaam.
            Vilevile kuna Mgogoro kati ya producer Man Walter na msanii 20 Percent uliopelekaea kusitisha kufanya kazi pamoja katika studio za Combination Sound chini ya Producer Man Walter hali iliyopelekea  msanii huyo kupotea katika ramani ya muziki.
            Asilimia 75 ya albamu ya msanii 20 percent iliyokwenda kwa jina la ‘yanini malubano’ na iliyojizolea umaarufu mkubwa hadi kupelekea kunyakua tuzo tano za kili music award nchini mwaka 2011 ilitengenezwa na producer huyo.
Mgogoro mwingine ulimuhusisha msanii Mrap na Producer Pancho latino kutoka katika studio za Bhits,kama ilivyowazi waliwahi kufanya kazi zikiwemo Attention na Destiny zote alimshirikisha msanii Deddy na ngoma kibao za dj choka na Bhits Group.
Pia kuna mgogoro uliowahi kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari ambao ulihusisha Bhits group(yaani wasanii wote waliokuwa lebel katika studio za Bhits) na producer Herm B kitu kilichofanya baadhi ya wasanii kupoteza mashabiki wao,baadhi ya wasanii waliokuwapo katika kundi ni kama Vannesa Mdee,Deddy,Mabeste,Mrap na Gosby ambao walifanya nyimbo ikiwemo ya ‘Latino Nation’ na vibao kadhaa vya Dj choka.