PRODUCER DUPY WA UPRISE MUSIC AJIPA TANO KUFANYA KAZI NA MASTER J

MWAANDAAJI wa muziki anayekuja kwa kasi katika gemu ya muziki wa kizazi kipya nchini,James Lilai maarufu kama Dupy amekiri kukua kimuziki kutokana na kufanya kazi kwa kushirikiana na nguli wa uandaaji wa muziki nchini,Master J
Producer Dupy

Akizungumza na MUZIKI BEGANI,alisema anajisikia mwenye furaha na amani moyoni mwake na ambaye kipaji chake kimeimarika kutokana na kufanya kazi na mkongwe huyo katika soko la muziki nchini .

producer Dupy  akiwa na Legendary Master J
Dupy alivuma kwa kutengeneza vibao kibao zilizotamba katika vyombo mbalimbali vya habari nchini kutoka katika studio yake vikiwemo,Tumoghele,haina kufeli,mr christmass na kidawa zote za Izzo Bizness,lango la jiji ya stamina, wimbo wa msanii young kacha na stuggling na Myself
              wimbo mpya wa izzo bizness ft shaa uliotengenezwa na waandaaji hao wawili