
Kanye West ameendelea kufumbua mafumbo kuhusu albam yake mpya iliyoko jikoni. Baada ya siku chache zilizopita kusema hatua ilipofikia kuelekea kukamilika (80%), rapper huyo sasa ametoa jina litakalobeba albam hiyo. Jumapili (March 1) Kanye alitweet ‘So Help Me God’, ‘New Album title…’ iliyoambatana na picha ambayo huenda ikawa artwork ya albam hiyo.