PichaZ: J.Martins kufanya collabo na Koffi Olomide




Staa wa Nigeria ambaye amewahi kufanya collabo na wasanii wa Tanzania AY na Ommy Dimpoz, J.Martins ameingia studio kufanya collabo na mkongwe kutoka D.R.C, Koffi Olomide.

 
Martins ameshare picha Facebook akiwa na legend huyo na kuandika ujumbe kuwa anaamini muziki ni kitu kinachotuunganisha Waafrika, hivyo Kazi yake ni kutengeneza muziki ambao utawaunganisha waafrika, na kuionesha dunia kuwa Afrika sio bara bali ni nchi inayozungumza lugha moja ambayo ni muziki.



“My mission is to make music that Unites us all as Africans. I beleive music is one big thing brings us all together to further show the world that AFRICA is not a continent.. Africa is a country and we all speak one language – MUSIC! Get ready for my collaboration with the Congolese legend Koffi Olomide. Spread your love for African Music by sharing the good news with your friends far and wide. One Love, One Africa!”



J.Martins mwanzoni mwa mwaka huu (2015) alitoa wimbo uitwao ‘Time is Now’ aliomshirikisha mkongwe mwingine wa Afrika, Youssou N’dour kutoka Senegal.