IDRISA AUMBUKA BAADA YA KUONGEA UONGO BIG BROTHER

Baada ya kuishiwa pointi ya kuchangia wakati wenzake wakizungumzia mpira wa miguu na jinsi nchi za Afrika zinavyoboroka katika mashindano ya kimataifa, mwakilishi wa Tanzania, Idris aliamua kutibua maongezi hayo kwa kusema Tanzania imewahi kucheza Kombe la Dunia.
Ni kama wenzake hawakumsikia vizuri au kumwelewa, lakini mshiriki kutoka Kenya aliguna na kumuuliza tena Idris arudie alichosema.
Kwa kujiamini Idris alisema Tanzania imewahi kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 1978. Hapo Alusa alikuja juu na kuanza kumzodoa Idris huku akimuuliza mara mbilimbili, Tanzania ipi iliyowahi kushiriki fainali hizo.
Huku akimfukuza mahali walipokaa, Alusa alimwambia: “Usiwadanganye Waafrika, Tanzania haijawahi kushiriki mashindano hayo, Idris usiwalishe pumba Waafrika.”

0 Response to "IDRISA AUMBUKA BAADA YA KUONGEA UONGO BIG BROTHER"

Chapisha Maoni