Wema Sepetu na MC Pilipili kufungua Kili Chat Show Alhamis, 16 October 13, 201


10251893_597395403720082_1307347307482626356_n
Muigizaji maarufu na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu pamoja na mchekeshaji aliyejizolea umaarufu, MC Pilipili, watakuwa mastaa wa kwanza kuonekana kwenye kipindi kipya cha TV, Kili Chat
Kili Chat ni kipindi kitakachokuwa kikienda sambamba na msimu wa pili wa kampeni ya ‘Nani Mtani Jembe’ na kitarushwa mara ya kwanza Alhamis ya October 16 saa 3 usiku kupitia kituo cha runinga cha EATV.
Mtangazaji wa show hiyo ni Gadner G Habash ambaye kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutangaza amekuwa na mashabiki wengi.
Wawili hao watapewa changamoto mbalimbali na mtangazaji wa kipindi hicho na kila mmoja atakuwa pale kutetea maslahi ya timu anayoishabikia, kati ya Simba au Yanga.

0 Response to "Wema Sepetu na MC Pilipili kufungua Kili Chat Show Alhamis, 16 October 13, 201"

Chapisha Maoni