KING MAJUTO NA UJIO MPYA KATIKA FILAMU NA WEMA NA DIAMOND NI SHEEEDAAAAHHH


Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, King Majuto amesema hivi kariburi alimshawishi Wema Sepetu azungumze na mpenzi wake Diamond Platnumz ili wafanye kazi ya pamoja.
Diamond na Mzee Mjuto
Mzee Majuto ambaye ni mshindi wa Tuzo za Watu 2014 ya filamu inayopenda, ameiambia Bongo5 kuwa amemwachia kazi hiyo Wema ili azungumzee na mzee (Diamond).

“Hivi karibuni nilikuwa na Wema, nimemwambia aongee na Diamond ili tufanye filamu ya pamoja,” amesema Majuto. “Mimi, Wema na Diamond, hata Diamond ninaweza kuzungumza naye sema nimeanza na Wema kwanza, akikubali mtasikia tu.”

Kwa upande mwingine Majuto amesema ili acheze filamu anahitaji kulipwa shilingi milioni 3.

“Umri unaenda sasa biashara za nisaidie nisaide hakuna, kama unanitaka ili tufanye kazi unatakiwa uandae milioni 3.”

0 Response to "KING MAJUTO NA UJIO MPYA KATIKA FILAMU NA WEMA NA DIAMOND NI SHEEEDAAAAHHH"

Chapisha Maoni