Nay Wamitego amuahidi kumuwekea dhamana Nash Mc baada ya kumkosha



Baada ya Nash Mc kuandika ujumbe kupitia kurasa yake ya Facebook kuhusiana na swala zima la Katiba Mpya ambayo imekabidhiwa kwa Mh. Rais Kikwete. Baadhi ya wasanii waliohudhuria Dodoma jana walikubaliana na Katiba hiyo na kusema haina tatizo kwa kuwa imegusa mambo yote yanayowasibu wasanii.


Nash ameandika hivi "Shirikisho la Wasanii na Wasanii nchini nimewasikia kwa masikio yangu na Wengine tumewaon
a Leo Dodoma wakisema kua Katiba mpya haina tatizo kwa kua imegusa mambo yote yaliyokua yanawasibu wasanii,sasa nikisikia msanii analalamika Mbele yangu na nilimshuhudia akiunga mkono katiba mpya sijui nitakachomfanya mtasikia nipo Segerea!
Haki ya Mungu na. Mtume!"



Nay Wamitego nae akapost akisema haya "Hahahaaa kusema kweli kabisaaaaaaaa weh jamaa umenikosha sana katika cku zoteeeee Mi nitakuja kukuwekea dhamana mwana!!! Umetishaaaa mnoooo

0 Response to "Nay Wamitego amuahidi kumuwekea dhamana Nash Mc baada ya kumkosha"

Chapisha Maoni