MWIGIZAJI MZEE MANENTO KUZIKWA KESHO MOSHI-KILIMANJARO

MSIBA : Muigizaji Mzee Manento amefariki dunia.

NA SYLVESTER DAVID
MAZISHI ya msanii wa filamu za Kibongo, Mzee Manento yanatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi nyumbani kwao mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na MUZIKI BEGANI Jana Jijini Dar es salaam,mmoja wasanii wa Bongo Movie anayetambulika kwa jina la, Robert Augustino maarufu kama Kiwewe alisema mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro baada ya kuuaga rasmi jana nyumbani kwake kigogo.

Manento alifariki dunia juzi akiwa amelazwa katika hospitari ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu.

Mzee Manento atakumbukwa sana kwenye ulimwengu wa filamu nchini kutokana na kuonesha mchango mkubwa katika filamu za kibongo kama 'Hero of the Church', 'Dar to Lagos', 'Fake Pastor' na nyinginezo.

 Ndugu, jamaa na marafiki kwa sasa wamekutana nyumbani kwa marehemu kujadili kuhusu taratibu za kumsafirisha marehemu na utaratibu mzima wa mazishi.

Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi. AMEEN!