Kama ilipangwa Sitti Abbas Mtemvu aibuka mshindi Redd's Miss Tanzania 2014,kujinyakulia milioni 18,mabango na vipeperushi vya ushindi vyatawala.! tazama pichaz na matukio


Baada ya kuibuka Mlimbwende kutoka kwa washiriki 30, Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akishuka jukwaani kwa ulinzi mkali wa mabaunsa.Sitti Mtemvu alianza kwa kunyakua Redds Miss Chang'ombe na baadaye Redds Miss Temeke. Sitti ni binti wa Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu.
 Baadhi ya washabiki na wapambe wa wakiwa na vipeperushi vilivyotengenezwa maalum kumshangilia  Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu mara baada ya kutangazwa 
Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili,Lillian Kamazima (kulia) na Mshindi wa Tatu,Jihhan Dimachk mara baada ya kutawazwa rasmi usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.Sitti Mtemvu alianza kwa kunyakua Redds Miss Chang'ombe na baadaye Redds Miss Temeke. Sitti ni binti wa Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu.

  Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu akizungumza jambo mbele ya wanahabari mara baada ya mtoto wake kutangazwa kuwa 
Redd's Miss Tanzania 2014
Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas akivalishwa taji.
 Pichani ni Washiriki waliochaguliwa kuingia kwenye hatua ya tano bora katika shindano la Redds Miss Tanzania 2014 linaloendelea hivi sasa ndani ya ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar.Picha zote na Othman Michuzi.
 Mmoja wa Washiriki waliongia katika nafasi ya tanno bora shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakijibu maswali mbalimbali
 Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya pichani kulia Ommy Dimpoz akitumbuiza jukwaani akiwa sambamba na msanii Vanessa Mdee mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani),waliofika kushuhudia shindano hilo.
Washiriki wa Redds Miss Tanzania 2014 wapatao 15 mara baada ya kuchujwa. 
 Sehemu ya baadahi ya Wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye shindano hilo la kumsaka Kinara wa Redds Miss Tanzania 2014 
Baadhi ya Washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakicheza moja ya onesho lao la ufunguzi wa shindano hilo,ambapo mshindi atatangazwa usiku huu na kujinyakulia kiasi cha shilingi miloni 18 taslim.
 Baadhi ya Washiriki wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014,wakiwa jukwaani na mavazi ya ufukweni. 
 Msaniii wa Muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee a.k.a V-Money akitumbuiza kwenye shindano la kumsaka mshindi wa Redds Miss Tanzania 2014,yanayofanyika usiku huu ndani ya moja ya ukumbi wa Mlimani,jijini Dar. 
 Washiriki wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakikatiza jukwaani na mavazi yao ya ubunifu
 Baadhi ya Majaji wakifuatilia kwa makini 
Pichani ni Washiriki wa Redds Miss Tanzania 2014 wapatao 30 wakiwa jukwaani tayari kwa kuanza kuchujwa kupata washiriki 15 bora. Picha zote na Othman Michuzi.

0 Response to "Kama ilipangwa Sitti Abbas Mtemvu aibuka mshindi Redd's Miss Tanzania 2014,kujinyakulia milioni 18,mabango na vipeperushi vya ushindi vyatawala.! tazama pichaz na matukio"

Chapisha Maoni