NAH REEL:NAVY KENZO HAIJAVUNJIKA MASHABIKI TEGEMEENI MAMBO MAZURI

http://www.bongossip.com/wp-content/uploads/2014/09/4705IMG-20140919-WA0002.jpg

NA SYLVESTER DAVID
MWANDAAJI wa muziki  na msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka katika kundi la Navykenzo ,Emanuel Mkono‘Nah Reel’amekanusha uvumi wa kuvunjika kwa kundi hilo.

Akizungumza MUZIKI BEGANI kuhusu kutoonekana katika mahojiano mbalimbali,matamasha na kazi zinginezo za kundi kwa msanii mmojawapo wa kundi hilo anayejulikana kama Weestar, alisema waliamua kumtoa kutokana na ushirikiano wake dhaifu katika kazi za  kundi.

“Navykenzo haijavunjika ila tuliamua kumtoa msanii Weestar kutokana na utendaji dhaifu katika kazi za kundi letu,ila kundi lipo na litazidi  kuwapa burudani mashabiki wake”.Alisema Nah Reel.

Vilevile Nah Reel alitaja baadhi ya sababu zilizomfanya Weestar kutolewa ni kutoendana kwa aina ya muziki wafanyao, kuchelewa kwenye maonesho mbalimbali ya kundi na kutohudhulia mazoezi.

Kundi hilo lililowahi kutamba na nyimbo kama,hold me back,usinibwage,I do work, Aiyola,Bokodo Chelewa, kwa asa limeachia kibao kipya kilichopokelewa vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari nchini kijulikanacho kama ‘I wanna love’.

Pia aliwataka mashabiki wa muziki nchini  wategemee kazi nzuri na zenye ubora kutoka Navykenzo ambazo zitawajia hivi karibuni.








0 Response to "NAH REEL:NAVY KENZO HAIJAVUNJIKA MASHABIKI TEGEMEENI MAMBO MAZURI"

Chapisha Maoni