NAH REEL:KUFANYA KAZI NA MASTAA KIBAO NCHINI NI KIPIMO CHA UWEZO WANGU


              Producer Nah Reel akiwa studio


NA SYLVESTER DAVID
MWANDAAJI maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini,Emanuel Mkono‘Nah Reel’amekiri kuwa na uwezo mkubwa katika uandaaji wa muziki kutokana na kazi alizozifanya na wasanii mbalimbali wakubwa nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na MUZIKI BEGANI  kuhusu mabadiliko ya muziki nchini,alisema mabadiliko ni makubwa sana na yuko katika hatua za kuleta muziki mzuri katika soko la muziki nchini.

Nah Reel ambaye ni mwandaaji aliyefanya kazi katika studio za Kama Kawa Record,Home Town Record,Switch Record na sasa katika studio yake ijulikanayo kama ‘The Industy’.

Aliwataja wasanii aliofanya nao kuwa ni   wengi wakiwemo Kundi la Weusi,Vanessa Mdee, Diamond Platnum,Bonta,Kundi la Navy Kenzo,Izzo Busness,Kundi La Pah One,Mwana Fa,Roma,Kalla Jelemaya,Baba Levo,Rama D,Mapacha(Maujanja Suplayaz),Gosby,Quick Racka na Shilole.


Pia aliwataka mashabiki wa muziki wake nchini  wategemee kazi nzuri na zenye ubora kutoka kwake na studio yake ya ‘The Industry’.

             PICHA ZA BAADHI YA WASANII ALIOWAHI FANYA NAO KAZI




         QUICK RACKA

                                                                                           DIAMOND 

                 IZZO BIZNESS

            SHILOLE

                       VANESSA MDEE

0 Response to "NAH REEL:KUFANYA KAZI NA MASTAA KIBAO NCHINI NI KIPIMO CHA UWEZO WANGU "

Chapisha Maoni